Harambee Starlets wapiga mazoezi ya kwanza Morocco, kujiandaa kwa WAFCON

Timu nne bora katika kipute hicho zitafuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya almaarufu Harambee Starlets, ilifanya mazoezi ya kwanza Ijumaa, kujiandaa kwa kipute cha mataifa ya Afrika-WAFCON,kuanzia Jumapili Julai 26.

Starlets wanaoshiriki WAFCON kwa mara ya pili katika historia watakuwa na lengo moja nchini Morocco,kuwa timu ya kwanza ya Kenya kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa watu wazima.

Vipusa wa kocha Beldine Odemba watashuka dimbani Rabat ,Jumapili usiku kwa mkwangurano wa ufunguzi kundini A, dhidi ya Atlas Lioness ya Morocco kuanzia saa tano usiku.

Mataifa mengine kundini A na Kenya ni Algeria na Senegal.

Timu nne bora katika kipute hicho zitafuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Share This Article