Wanyamapori wafariki kutokana na kimeta DRC

Kulingana na maafisa wa mbuga hiyo, ugonjwa huo ulisababisha vifo vya viboko 28 ndani ya muda wa mwezi mmoja.

Tom Mathinji
1 Min Read
Ugonjwa wa kimeta (Anthrax) wasababisha vifo vya wanyamapori DCR.

Huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ikiendelea kupambana na msambao wa ugonjwa wa Ebola, wanyamapori katika mbuga ya kitaifa ya Virunga wako katika hatari ya kuangamia, kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kimeta (Anthrax).

Katika muda wa wiki kadhaa zilizopita, mizoga ya viboko imegunduliwa katika mto Semuliki iliyo kwenye mbuga hiyo ambayo ni ya zamani sana katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika, na kuibua wasiwasi miongoni mwa jamii.

“Katikati ya mwezi Septemba, tulianza kugundua mizoga ya viboko kwenye mto Semuliki. Tulianza kupata hofu kuhusu hali hiyo, huku tukikabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola,” alisema mkazi mmoja wa eneo la  Vitshumbi.

Uchunguzi wa maabara uliotekelezwa na mbunga ya kitaifa ya Virunga, ulithibitisha kuwa viboko hao walifariki kutokana na maambukizi ya kimeta.

Kulingana na maafisa wa mbuga hiyo, ugonjwa huo ulisababisha vifo vya viboko 28 ndani ya muda wa mwezi mmoja.

“Ugonjwa huu unaweza ambukizwa mwanadamu iwapo atatangusana na mizoga ya wanyama, wanyama walioambukizwa au kula nyama iliyoambukiwa ugonjwa huo,” ilisema taarifa kutoka kwa mbuga hiyo.

TAGGED:
Share This Article