Kampuni ya bima ya Jubilee imemteua Juan Cazcarra kuwa Afisa Mkuu Mtendaji kuanzia Disemba mosi mwaka huu.
Cazcarra anamrithi Dr. Julius Kipng’etich, ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu mwaka 2018, na atastaafu rasmi tarehe 30 mwezi huu.
Juan ana tajiriba ya zaidi ya miaka 20 katika sekta ya bima baada ya kusimamia sekta hiyo katika mabara ya Ulaya, Asia na Afrika.
Juan alijiunga na Jubilee Group mwezi Julai mwaka 2021 na kuteuliwa naibu Afisa Mkuu Mtendaji tangu mwezi Aprili mwaka 2025.