Waziri wa afya Aden Duale siku ya Jumatatu ametukana na viongozi wapya waliochaguliwa maajuzi wa Baraza la Magavana nchini (CoG) katika makao makuu ya Wizara .
CoG ikiongozwa na mwenyekiti mpya ambaye pia ni Gavana wa kaunti ya Tharaka Nithi Muthomi Njuki, ilijadailiana na Duale kuhusu majukumu ya kaunti katika ufanisi za sekta ya afya nchini.
Mazungumzo hayo yalijikita katika mradi wa kutengeza miwani ya macho wa Presbyopia ambao unanuiwa kutekelezwa katika kaunti saba nchini kwa ushirikiano na wafadhili wa kimataifa .
Aidha,walijadiliana kuhusu utekelezaji wa afya kwa wote nchini UHC ,kuendeleza Taifa Care,kuboresha afya ya msingi na utekelezaji wa mfumo wa habari kuhusu afya.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu wa huduma za matibabu Dkt. Ouma Oluga,Mkurugenzi Mkuu wa Afya Dkt.Patrick Amoth miongoni mwa viongozi wengine kutoka CoG na wizara.