Mabingwa watetezi Hellen Obiri na Benson Kipruto wataongoza wanariadha wa Kenya watakaotimka makala ya 56 ya mbio za New York City Marathon Jumapili jioni nchini Marekani.
Obiri aliyeweka rekodi mpya mwaka jana ya saa 2 dakika 19 na sekunde 51, analenga taji ya tatu ya mbio hizo baada ya kutwaa ubingwa mwaka 2023 na mwaka 2025.
Obiri atakabiliana na wenzake Sheila Chepkirui,Viola Cheptoo na Edna Kiplagat.
Kipruto aliyetwaa ushindi mwaka jana analenga kutetea taji hiyo inagawa atakuwa na kibarua cha ziada kutoka kwa bingwa wa zamani Geofrey Kamworor wa na Abdelaaye Negeeye na Cybrian Kotut.