Betty Chelangat na Cornelius Konori ndio washindi wa makala ya kwanza ya mbio za kilomita 10 za benki ya Absa kuadhimisha karne moja tangu wafungue tawi la Eldoret ,zilizoandaliwa mapema Jumapili.
Chelangat aliziparasaka kwa muda wa dakika 34 sekunde 43.7,akifuatwa na Leah Jekwmoi kwa dakika 34 sekunde 49.5, huku Sharon Kiptugen akiridha nafasi ya tatu.
Cornelius Kipkosgei Konor alitwaa ubingwa wa mbio za wanaume kwa kutumia dakika 30 sekunde 27.4,mbele ya David Korichei na Mark Kipkoech, walioambatana katika nafasi za pili na tatu kwa dakika 30 sekunde 34.8, na dakika 30 sekunde 36.5 mtawalia.
Mbio hizo zilikamisliha wiki moja ya sherehe za kuadhimisha karne moja tangu kuanzishwa kwa benki mjini Eldoret.