Idadi ya maafa kutonakana na Ebola yafika 5,000 DRC

Hadi kufika sasa hakuna chanjo ambayo imeidhinishwa kwa matibabu ya ugonjwa huo aina ya Bundibugyo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Idadi ya vifo kutokana na Ebola imefika 5,000 nchini DRC.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imefika 5,000, kulingana na takwimu iliyotolewa na serikali siku ya Ijumaa.

Serikali ya DRC kwa ushirikiano wa washirika wa kimataifa , zinajizatiti kukabiliana na msambao wa ugonjwa huo hatari, huku maambukizi ya ugonjwa huo yakifika 10,000 tangu ugonjwa huo kuzuka katika taifa hilo.

Hadi kufika sasa hakuna chanjo ambayo imeidhinishwa kwa matibabu ya ugonjwa huo aina ya Bundibugyo.

Hata hivyo ugunduzi wa ugonjwa huo ukiwa umechelewa, ghasia na huduma hafifu za afya, umechangia kuenea kwa ugonjwa huo hadi mikoa nane kati ya 26 kufikia sasa.

Ugonjwa huo umeenea pia katika nchi jirani, Nigeria ikiwa taifa la hivi karibuni kutangaza maambukizi ya Ebola.

Kenya na Uganda pia zimenakili maabukizi ya ugonjwa huo, lakini Uganda ilitangaza kumalizika kwa maambukizi ya Ebola nchini humo.

TAGGED:
Share This Article