Kompany anapokea matibabu baada ya kuzirai

Makocha wasaidizi wa Kompany watasimamia mazoezi na mechi za klabu hiyo kwa muda hadi hali yake itakapokuwa shwari.

Dismas Otuke
0 Min Read

Meneja wa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich Vincent Kompany anapokea matibabu hospitalini baada ya kuanguka na kuzirai wakati wa mazoezi ya timu ya akiba siku ya Ijumaa.

Kompany anapokea vipimo kadhaa hospitalini na atasalia chini ya uangilizi wa madaktari.

Makocha wasaidizi wa Kompany watasimamia mazoezi na mechi za klabu hiyo kwa muda hadi hali yake itakapokuwa shwari.

Share This Article