Ruto kuzuru Ukambani kwa ziara ya siku nne kuanzia Jumamosi

Dismas Otuke
1 Min Read
William Ruto- Rais wa Kenya.

Rais William Ruto atazuru kaunti za Ukambani kwa ziara ya siku nne kuanzia Jumamosi hii kukagua miradi ya maendeleo na kuanzisha miradi mipya.

Miradi atakayokagua na kuzindua katika kaunti tatu za Ukambani za Machakos,Makueni na Kitui ni pamoja na barabara,nyumba za gharama nafuu,uunganishaji umeme na miradi ya maji hali kadhalika utoaji hatimiliki za ardhi.

Rais ataanza ziara yake eneo la Mbiuni eneo bunge la Mwala kaunti ya Machakos, kabla ya kuelekea Mbooni kaunti ya Makueni.

Baadaye atazuru Ilima kutoa hati miliki za ardhi na kumalizia kaunti ya Makueni Jumamosi jioni.

Jumapili Rais ataendeleza ziara katika kaunti ya Makueni, kabla kufanya ziara nyingine huko Kitui na Makueni siku ya Jumatatu.

Jumannne Ruto atatembelea maeneo ya Mwingi Kaskazin kaunti ya Kitui,Masinga na Yatta kaunti ya na kumalizia Matuu .

Share This Article