Dereva wa basi ashtakiwa kwa kusababisha mauaji

Wanjala aliyefikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya Nyando Evelyn Makungu Onzere, alikanusha mashtaka hayo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Dereva wa basi afunguliwa mashtaka kwa kusababisha mauaji.

Dereva wa basi amefunguliwa mashtaka kwa kusababisha mauaji ya wanafunzi wawili wa Chuo cha Kiufundi cha Mombasa, kwenye ajali ya barabarani iliyotokea Agosti 7, 2026, kwenye Barabara Kuu ya Ahero-Awasi kaunti ya Kisumu.

Jotham Murumba Wanjala, alifunguliwa mashtaka 12, mawili yakiwa ni ya kusababisha vifo kupitia uendeshaji hatari wa gari, uliosababisha vifo vya Evance Odiwour Otieno na Rooney Owek Gakumba.

Hata hivyo, Wanjala aliyefikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya Nyando Evelyn Makungu Onzere, alikanusha mashtaka hayo.

Kulingana na upande wa mashtaka, Wanjala aliendesha basi hilo kwa kasi na mwenendo ambao ulihatarisha maisha ya umma, kabla ya kupotesha mwelekeo na kusababisha ajali hiyo.

Mahakama ilimwachiliwa Wanjala kwa dhamana ya shilingi 500,000, kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa Novemba 5, 2026.

TAGGED:
Share This Article