Ruto amkabidhi Mnangagwa uongozi wa COMESA

Upande wake Mnangagwa amesema jukumu lake la kwanza afisini ni kudumnisha ufanisi ulioafikiwa kufikia sasa na pia kuafikia ruwaza yake.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya imekabidhi rasmi uenyekiti wa soko la pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) kwa Zimbabwe, wakati wa kongamo la 25, lililoandaliwa Alhamisi mjini Harare Zimbabwe.

Rais William Ruto akihutubia kongamano hilo amesema ana imani kuwa mrithi wake ataafikia ruwaza ya COMESA ya kuwa na soko dhabiti na ustawi wa muungano huo.

Ruto alisema haya akikabidhi Uenyekiti wa COMESA kwa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, akikamilisha mwaka mmoja ambapo amekuwa Mwenyeki wa muungano.

Upande wake Mnangagwa amesema jukumu lake la kwanza afisini ni kudumnisha ufanisi ulioafikiwa kufikia sasa na pia kuafikia ruwaza yake.

Share This Article