Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, ametaka uwajibikaji, usimamizi jumuishi na uwakilishi zaidi wa mashirika ya kimataifa ili kurejesha imani ya umma.
Akizungumza katika siku ya pili ya kongamano la kimataifa la uaminifu maarufu kama Global Trust Summit Jijini Nairobi, Mudavadi aliongeza kuwa imani ya umma haiwezi kuwepo bila maadili.
Aliongeza kuwa Imani na uwajibikaji vinapaswa kuambatana, ili kurejesha uaminifu wa umma.
Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, alikubaliana na kuunga mkono ripoti ya kimataifa ya mwaka 2026, iliyosema kuwa Imani ya umma imeshuka kutoka asilimia 42 mwaka 2018, hadi asilimia 37 mwaka 2025.