Rais Ruto kukabidhi Uenyekiti wa COMESA kwa Mnangagwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto aliye ziarani nchini Zimbabwe anatarajiwa kukabidhi Uenyekiti wa soko la pamoja kwa mataifa ya mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) wakati wa kongamano la 25 siku leo Alhamisi.

Ruto atamkabidhi Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kuwa mwenyekiti wa COMESA baada ya kukamilisha muda wake wa kuhudmu wa mwaka mmoja.

Ruto aliwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Robert Gabriel Mugabe Jumatano jioni kujiunga na viongozi wengine tayari kwa kongamano la COMESA.

Kenya ilitwaa Uenyekiti wa Comesa kutoka kwa Burundi mwaka 2025, wakati wa kongamano la 24 lililoandaliwa mjini Arusha,Tanzania.

Kongamano hilo linaleta pamoja wanachama 21 kujadiliana kuhusu bishara za kikanda,viwanda,uekezaji pamoja na ustawi wa pamoja wa kiuchumi.

Share This Article