Matumaini ya Tusker FC kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika yamedidimia baada ya kulazwa nyumbani bao moja kw abila na wageni Singinda Black Stars ya Tanzania.
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo Jumapili alasiri .
Singida walijipatia bao pekee na la ushindi kuanko dakika za mwisho mwisho za mechi hiyo kupitia kwa wing’a wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jeancy Mboma.
Tusker ni sharti sasa washinde mkumbo wa pili mabao 2-0 wiki ijayo ili kufuzu kwa hatua ya makundi.