Mashindano ya riadha ya Ultimate kuanza leo Ijumaa mjini Budapest

Makala ya kwanza ya mashindano mapya ya Riadha duniani ya Ultimate Championship, yataanza leo Ijumaa Septemba 11 na kukamilika Jumapili hii mjini Budapest,Hungary.

Dismas Otuke
1 Min Read
Emmanuel Wanyonyi baada ya kushinda taji ya Diamond-Picha hisani-Aaron Bui

Makala ya kwanza ya mashindano mapya ya Riadha duniani ya Ultimate Championship, yataanza leo Ijumaa Septemba 11 na kukamilika Jumapili hii mjini Budapest,Hungary.

Wanariadha 14 wa Kenya ni miongoni mwa wanariadha 381 kutoka mataifa 65, wanaotarajiwa kushiriki .

Bingwa wa Dunia mwaka 2019 Timothy Cheruiyot, atatimka mita 1,500 pamoja na Phanuel Kosgei.

Mbio za mita 5,000 zitashuhudia Jaco Krop na Cornelius Kemboi wakishiriki,wakati bingwa wa Olimpiki Emmanuel Wanyonyi akitimka mita 800 naye bingwa wa Afrika Julius Yego,  atashiriki urushaji sagai.

Aidha,Mercy Oketch, atakimbia mita 400, huku pia kijumuishwa katika timu ya mita 400 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti mseto.

Kenya itawakilishwa na timu ya mita 400, inayowajumuisha George Mutinda,Boniface Mweresa,Kelvin Kiprotich na Lanoline Aoko.

Mashindano hayo ambayo  yatakuwa na donge nono la pesa la kima cha shilingi bilioni  1.3, huku mabingwa  wa kila  mabingwa wa kila fani wakituzwa shilingi milioni 19.4

Mashindano hayo yanawashirikisha mabingwa wa Olimpiki,Mabingwa wa Dunia na mabingwa wa Diamond League katika fani 28 tofauti.

Share This Article