Shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) linatarajiwa kunufaika pakubwa kutokana na hatua ya shirikisho la kandanda Afrika (CAF) kutangaza kuongeza mgao wa kila mwaka kwa mashirikisho kwa hadi asilimia 33.
FKF ambayo hupokea shilingi milioni 68.2, sasa itapokea shilingi milioni 90.9, kwa mwaka kutoka kwa CAF,ili kufadhili miradi ya maendeleo ya soka humu nchini.
Rais wa CAF Patrice Motsepe amefichua kuwa kila shirikisho kati ya mashirikisho yote 54 ya Afrika, litapokea mgao huo wa shilingi milioni 90.9.
Aidha,FKF itapokea kitita kingine cha shilingi milioni 22.7, kutoka kwa CAF, kugharamia usimamizi,kuimarisha usimamizi na kuimarisha utendakazi wake.
CAF ilianza kutoa fedha hizo kwa mashirikisho mwaka 2021 ambapo kila shirikisho lilikuwa likipokea shilingi milioni 25.9 kwa mwaka.