Rais Ruto atia sahihi miswada miwili kuwa sheria katika Ikulu ya Eldoret

Sheria hizo zinaongeza muda wa kupunguza ushuru wa thamani yaani VAT kwa bidhaa za Petroli kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8 kwa kipindi cha siku 90 zaidi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ametia sahihi kuwa sheria misuada miwili ikiwemo ile ya kufanyia marekebisho sheria za ushuru yaani Tax Laws (Amendment) Bill ya mwaka 2026, na ile mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini yaani Kenya Revenue Authority (Amendment) Bill ya mwaka 2026 kuwa sheria.

Hafla hiyo imeandaliwa mapema Ijumaa katika Ikulu ndogo ya Eldoret kaunti ya Uasin Gishu.

Sheria hizo zinaongeza muda wa kupunguza ushuru wa thamani yaani VAT kwa bidhaa za Petroli kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8 kwa kipindi cha siku 90 zaidi.

Aidha,sheria ya pili ya KRA iliyosainiwa na Rais inawezesha kupunguza kwa ushuru wa unaotozwa vigae vya ujenzi,bidhaa za usafi na glasi za ujenzi ili kupunguza gharama ya ujenzi,na kuongeza fursa za ajira.

Share This Article