Mbunge wa binge la Afrika Mashariki (EALA) Winnie Odinga, ametangaza kuwania kiti cha Seneta wa gatuzi la Nairobi katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Odinga alifichua hayo siku ya Alhamisi katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha babake,Raila Odinga mjini Bondo kaunti ya Siaya.
Alisema kuwa analenga kufanya kazi kwa karibu na vijana wa kaunti ya Nairobi endapo atachaguliwa.
Odinga alisema amechochewa kugombea Useneta na Seneta anayeondoka Ewdwin Sifuna, ambaye ameonyesha azma ya kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa upinzani wakiwemo Edwin Sifuna,Kalonzo Musyoka na Martha Karua.