Harusi ya Diana na Bahati : Viti 67 vyasalia

Wanahimiza yeyote anayetaka mwaliko, awawapigie simu.

Marion Bosire
2 Min Read

Wanandoa na wanamuziki nchini Kenya Diana Marua na Bahati wanaendelea na mipango ya harusi yao ya kifahari, huku wakiendelea kuuza mialiko.

Mwaliko mmoja wa hafla hiyo unauzwa shilingi milioni 1 pesa za Kenya na kufikia sasa wamefanikiwa kuuza mialiko 33, kutokana na mialiko jumla ambayo ni 100 pekee.

Hivi leo wawili hao wamechapisha picha ya pamoja kuhusu hafla ijayo na kuandika, “Haya mapenzi yamedumu Kama Petfume ya Woria. Viti 67 vimesalia katika siku kuu ya The Bahatis”,

Waliongeza ujumbe kwamba yeyote anayetaka mwaliko, ana uhuru wa kuwapigia simu na kuupata kwa shilingi milioni moja pekee!

Bahati ameonyesha hadharani akiwapa mialiko Mhubiri tata Victor Kanyari na Kenyan Prince anayejihusisha na biashara ya ubadilishanaji wa fedha za kigeni.

Diana naye ameonyesha akiwapa mialiko Purity anayefanya biashara ya kuuza pazia na Damaris wa Dama Mobile Spares.

Mashabiki wa wawili hao sasa wanasubiri kuona iwapo hafla hiyo itafanikiwa au la huku wengi wakikosoa kiwango cha juu cha fedha zinazolipiwa mialiko.

Bahati na Diana walipatana mwaka 2016 kabla ya kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kufikia sasa wana watoto watatu pamona huku Bahati akiwa na binti mmoja mkubwa aliyepata na mtu mwingine kabla ya kuwa na Diana na wanalea pia kijana mkubwa aliyekuwa chini ya malezi ya Bahati hata kabla hajakutana na Diana.

Share This Article