EPRA yaongeza bei za mafuta

Bei ya petroli itaongezeka kwa shilingi 12.93, dizeli kwa shilingi 9.90 na mafuta taa kwa shilingi 28.49.

Tom Mathinji
1 Min Read
EPRA yaongeza bei za mafuta.

Halmashauri ya kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA), imetangaza nyongeza ya bei za mafuta, ikitaja hatua hiyo imetokana na kuongezeka kwa bei za mafuta yaliyoagizwa.

Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa Jumatano jioni, bei ya petroli itaongezeka kwa shilingi 12.93, dizeli kwa shilingi 9.90 na mafuta taa kwa shilingi 28.49.

Mabadiliko hayo yatatekelezwa Oktoba 15, 2026.

Kulingana na EPRA, bei hizo mpya zinajumuisha asilimi 8 ya ushuru ziada (VAT), ambayo serikali ilianza kutekeleza mwezi Aprili mwaka huu, kuwaokoa watumizi dhidi ya bei ghali zinazosababishwa na taharuki inayoshuhudiwa Mashariki ya Kati.

Lita moja ya mafuta ya petroli sasa itauzwa shilingi 226.96, dizeli shilingi  227.76 na mafuta taa shilingi 219.87.

Mabadiliko hayo yatasababisha gharana ya maisha kupanda kutokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa.

TAGGED:
Share This Article