Tusker FC waishika mateka Ulinzi Stars ,Ligi kuu Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Kombe la Mozzart Tusker FC wameanza vyema msimu wa mwaka 2026/2027 wa Ligi Kuu ya Sportspesa kufuatia ushindi wa mabao 2-0, ugenini dhidi ya Ulinzi Stars, katika mojawapo wa mechi nne zilizochezwa Jumapili.

Baada ya kipindi cha kwanza kumalizikia sare tasa Tusker walichukua uongozi kunako dakika ya 60 kupitia kwa Alvin Mang’eni, kabla ya Victor Mbaoma, kuongeza la pili dakika ya 75.

Mechi nyingine  tatu za Jumapili zilimalizia sare 3K FC wakitoka sare ya 2-2 na Mara Sugar,Migori Youth pia watoka sare ya 1-1 na Police FC, huko Awendo Green nao Nairobi United na Kenya Commercial Bank ,wakiambulia sare ya 2-2.

 

Share This Article