Bingwa Boston marathon mwaka huu Sharon Lokedi na Amos Kipruto aliyemaliza wa pili mwaka jana watarejea kutimika makala ya mwaka huu ya mbio za Chicago Marathon nchini Marekani leo jioni.
Lokedi atashirikiana na mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia Brigid Kosgei,Briallian Kipkoech,Loice Chemnung,Joan Kilimo,Magdalene Maasai na Mary Ngugi Cooper.
Ushindani unatarajiwa kutoka kwa bingwa mtetezi Hawi Feysa wa Ethiopia.
Kipruto atatimka mbio za wanaume akishirikiana na Daniel Mateiko, huku wakipata upinzani kutoka kwa bingwa mtetezi Jacob Kiplimo wa Uganda na Waethiopia Milkesa Mengesha na Tadese Takele Bikila.