Matabibu waliomuuguza mgonjwa wa Ebola walalamikia kunyanyaswa

Wanasema badala ya kutengwa kulingana na kiwango cha kutangamana na marehemu ,wanajumuishwa tu pamoja hali inayohatarisha maisha yao zaidi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Madaktari na wauguzi waliomhudumia mgonjwa wa Ebola aliyefariki katika hospitali ya Nairobi, wanalalamikia kunyanyaswa wakiwa baadhi ya waliokaribiana na marehemhu.

Madaktari hao  na wauguzi wanane wanasema walazismihwa kujitenga katika chumba alichofariki mgonjwa huo bila utarabu maalum kufuatwa licha ya wao wenyewe kujitambulisha.

Wanasema badala ya kutengwa kulingana na kiwango cha kutangamana na marehemu ,wanajumuishwa tu pamoja hali inayohatarisha maisha yao zaidi.

Aidha,wanasema ni makosa na kinyume cha taaluma kwa washukiwa wa kwanza waliotangamana kwa karibu na mgonjwa aliyefariki pamoja na wale ambao walitangamana na marehemu kwa umbali.

Wanaongeza kuwa wengi wanachukuliwa kama washukiwa wa makosa ya jinai katika mchakato wa kufanyiwa karantini.

Share This Article