Timu ya taifa ya soka ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17 ,Junior Starlets imewasili Morocco, Alhamisi jioni tayari kwa fainali za Kombe la Dunia.
Starlets wamekuwa kwa kambi ya siku nne nchini Uhispania kujiandaa kwa michuano hiyo itakayoanza tarehe 17 na kukamilika Novemba 7.
Kocha wa Kenya Mildred Omari alitangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 25 kwa kipute hicho.
Starlets watafungua kampeni dhidi ya Uchina tarehe 17 mwezi huu, kabla ya kukabiliana na Marekani Oktoba 22, na hatimaye dhidi ya Samoa siku tatu baadaye katika mechi za kundi E.
Kenya inashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya pili tangu ilipofuzu mwaka 2024 katika Jamhuri ya Dominika.