Kenya haina mlipuko wa Ebola, asema Muthoni

Mgonjwa mmoja rai wa Kenya aliripotiwa kufariki mapema wiki hii punde baada ya kuwasili nchini kutoka DRC kupitia uwanja wa JKIA.

Dismas Otuke
1 Min Read

Katibu wa Wizara ya Afya ya Umma Mary Muthoni amesema kuwa licha ya kisa cha kwanza cha Ebola kuripotiwa, Kenya haina mlipuko wa ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo.

Muthoni alitoa hakikisho hilo jana Jumatano jioni alipozuru Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA kutathmini hali ilivyo kwa abiria wanaowasili na wanaoondoka nchini.

Alidokeza kuwa hatua za tahadhari zimechuliwa za kukabiliana na maambukizi yoyote yatakayoripotiwa.

Aliongeza kuwa lango nambari 16 katika uwanja wa JKIA limetengewa wasafiri wanaowasili humu nchini kutoka mataifa kumi yaliyo na visa vingi vya Ebola yakiwemo DR Congo, Uganda, Tanzania, Ethiopia, Angola, Zambia, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini.

Aidha, Katibu huyo alitoa tarakalishi na vitakasa mikono ili kusaidia katika uchunguzi wa abiria na kudumisha usafi kwa wanaowasili nchini.

Mgonjwa mmoja rai wa Kenya aliripotiwa kufariki mapema wiki hii punde baada ya kuwasili nchini kutoka DRC kupitia uwanja wa JKIA.

Share This Article