Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Junior ametoa wito wa hatua za kupambana na msambao wa ugonjwa wa Ebola kuimarishwa zaidi.
Ameonya kuwa Makueni hasa inaweza kuwa katika hatari ya kuathiriwa na ugonjwa huo kwa sababu ipo karibu na barabara kuu ya Nairobi-Mombasa.
Gavana Mutula sasa anatoa wito kwa serikali kuu, kupitia kwa Waziri wa Afya Aden Duale, kuimarisha uangalizi na hatua za kuzuia ugonjwa huo kwenye barabata hiyo ili kupunguza hatari ya kuenea kwake.
Amesema idadi kubwa ya watu wanaotumia barabara hiyo kusafiri kunafanya maandalizi na mwitiko wa mapema kuwa hata muhimu zaidi.
Gavana Mutula aliyasema hayo katika eneo la Uvete huko Kilome wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika wadi ya Mukaa.
Hadi kufikia sasa, Kenya imethibitisha kisa kimoja cha ugonjwa wa Ebola.