Mwandishi na mwanasiasa wa zamani wa Uingereza Jeffrey Archer amefariki

HarperCollins ambaye ni  mchapishaji wa vitabu vya Archer,  alisema mwandishi huyo alifariki ghafla akiwa nyumbani kwake siku ya Jumatatu.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwandishi na mwanasiasa wa zamani Jeffrey Archer amefariki.

Mwandishi wa vitabu na mwanasiasa wa zamani wa Uingereza Jeffrey Archer, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 86.

Kupitia kwa taarifa, HarperCollins ambaye ni  mchapishaji wa vitabu vya Archer,  alisema mwandishi huyo alifariki ghafla akiwa nyumbani kwake siku ya Jumatatu.

Archer ameuza zaidi ya nakala 300 za vitabu alivyoandika katika taaluma yake ya uandishi ya miongo mitano, miomgoni mwa vitabu vyake ikiwa ni pamoja na Clifton Chronicles na Kane and Abel.

Mbunge huyo wa zamani wa chama cha Conservative aliyewakilisha eneo bunge la Lincolnshire, aliwahi hukumiwa gerezani kwa muda wa miaka minne kwa kosa la kutoa ushahidi wa uwongo.

Archer alizaliwa London Kaskazini April 15, 1940 na mwaka  1969, alichaguliwa mbunge, wadhifa alioushikilia kwa muda wa miaka tano, kabla ya kuchaguliwa kuwa naibu mwenyekiti wa chama cha Conservative.

Share This Article