Watu 30 wamefariki na wengi wengi kutoweka, kwenye ajali ya mashua katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kulingana na maafisa nchini humo, ajali hiyo ilitokea kwenye mto Congo Jumapili jioni karibu na eneo la Ngombe-Lukolela, mkoa wa Equateur, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, na kwamba juhudi za kuwatafuta waliopotea zinaendelea.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Mkoa wa Equateur Crispin Mputu, alisema mashua moja kwa jina ‘Dieu se cache,’ ilikuwa ikisafiri kutoka Jiji Kuu Kinshasa, ilipogongana na mashua nyingine kwa jina ‘HB Super Victoire,’ iliyokuwa ikisafiri kutoka Businga.
“Abiria wote walinaswa ndani ya maji, huku mashua hizo zikizama,” alisema afisa huyo.
Aidha, Mputu alithibitisha kuwa, wale wote walikufa maji tayari wamezikwa, akisema chanzo cha ajali hiyo hakijabainika.
Afisa mmoja wa usalama aliyeshuhudia ajali hiyo, alisema mashua iliyokuwa ikisafiri kutoka Kinsasha, ilikuwa imebeba abiria na mizogo kupita kiasi.