Rais wa Shirika la Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli (WADA) Witold Bańka, yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu.
Bańka alitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA mapema Jumapuli na anatarajiwa kukutana na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.
Pia anatarajiwa kukutana na viongozi wa Kamati ya Olimpiki nchini, NOCK siku ya Jumanne kabla ya kuwahutubia wanahabari.
Bańka anatarajiwa kutathmini maendeleo yaliyopigwa na Kenya kupitia kwa Shirika la Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli nchini (ADAK).
Aidha, kiongozi huyo anatarajiwa kufanya kikao na wanamichezo na maafisa wakuu serikalini.