Rais Ruto akamilisha utoaji hati miliki 300,000 pwani

Ruto amesema kuwa hatimiliki hizo zitahakikisha wakazi wanaishi bila hofu ya kutimuliwa kutoka kwa makazi yao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amekamilisha zoezi la wiki moja la utoaji hati miliki za ardhi 300,000 katika ukanda wa pwani.

Rais amekamilisha zoezi hilo siku ya Jumamosi kwa kutoa hati miliki 4,500 mjini Garsen kaunti ya Tana River.

Jumla ya hati miliki laki tatu zimetolewa kwa wamiliki wa ardhi katika uaknda wa pwani ndani ya kipindi cha siku nane ambazo Rais Ruto amekuwa eneo hilo.

Ruto amesema kuwa hatimiliki hizo zitahakikisha wakazi wanaishi bila hofu ya kutimuliwa kutoka kwa makazi yao.

Aliongeza kuwa serikali inadhamiria kutoa hati miliki nusu milioni ifiakipo disemba mwaka huu na pia itanunua ardhi kutoka kwa wastawishaji wa kibinasfi ikiwemo ekari kumi kutoka kwa Wachu na kiasi sawa na hicho kutoa kwa Haganda na ekari nyingine 5,000 kila moja kutoka kwa Kibusu na Kitangale ili kuwagawia Maskwota.

Aliahidi kurejea eneo hilo na kutoa hati miliki nyingine laki mbili ndani ya kipindi cha miezi miwili ili kumaliza tatizo la Uskwota katika eneo la pwani.

Share This Article