Rais wa Shirikisho la kupambana na ulaji muku ulimwenguni (WADA) Witold Banka atawasili nchini Kenya mapema Jumapili ambapo anatarajiwa kutathmini hatua zilizopigwa na Kenya kukabiliana na dawa za kututumua misuli.
Kando na kukutana na viongozi wakuu wa serikali ya Kenya Witold atahutubia Wanahabari siku ya Jumanne .
Haya yanajiri huku Kenya ikisalia katika orodha ya mataifa yanayochunguzwa kwa karibu na WADA kuhusiana na kuwa na visa vingi vya wanariadha wanaotumia dawa za kututumua misuli.