Moto mkubwa umezuka katika kijiji cha Mayanja Jumapili alasiri baada ya lori la mafuta kupata ajali na kupinduka katika barabara ya Bungoma-Malaba.
Inaaminika moto huo ulizuka baada ya mamia ya raia kufika eneo la ajali na kuasa kuteka mafuta kwa kutumia mitungi.
Moto huo umzsababisha msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo huku maafisa wa uokoaji kutoka shirika la msalaba mwekundu wakifika kuwasaidia majeruhi .
Mkasa huo umetokea karibu na shule ya upili ya Paul Boit High katika barabara kuu ya Eldoret-Turbo.
Haya yanajiri wiki moja tu baada ya watu watatu kufariki na wengine 23 kupata majeraha ya moto baada ya lori la mafuta kupata ajali na kulipuka moto wakati wakazi walijaribu kuteka mafuta.