Mabingwa wa Dunia Uhispania waizima Uingereza

Ushindi huo umefikisha mechi 39 ambazo Uhispania wamecheza bila kushindwa ikiwa rekodi mpya ya ulaya.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Dunia Uhispania walitoka nyma na kupata ushindi mabao 3-2 ugenini dhidi ya Uingereza, katika mechi ya kwanza kuwania Kombe la ligi ya mataifa ya Ulaya uwanjani Wembley nchini Uingereza Jumamosi usiku.

Ushindi huo umefikisha mechi 39 ambazo Uhispania wamecheza bila kushindwa ikiwa rekodi mpya ya ulaya.

Lamine Yamal alitumia makosa ya beki Marc Guehi kunako dakika ya pili na kupachika bao la kwanza kabla ya Anthony Gordon kukomboa kwa Three Lions dakika ya 36, naye nahodha Harry Kane akafunga la uongozi kwa Uingereza muda mfupi kabla ya mapumziko.

Kane alipoteza fursa ya kutanaua uongozi wa Uingereza alipopiga mlingoti wakati wa kupiga penati ya mwanzoni mw akipindi cha pili.

Nguvu mpya Alex Baena na Mikel Oyarzabal walijumuishwa uwanjani na kufunga bao moja kila moja .

Share This Article