Kiwanda cha kusafisha mafuta Lamu kuzalisha megawati 1,000 za umeme

Dangote alisema haya Ijumaa alipomwalika Rais William Ruto katika kiwanda cha kusafidha mafuta mjini lagos nigeraia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote amefichua kuwa kiwanda cha kusafisha mafuta kitakachozinduliwa wiki ijayo mjini Lamu kitazalisha megawati 1,000 za umeme huku kiasi cheke kikisambizwa serikali ya Kenya.

Dangote alisema haya Ijumaa alipomwalika Rais William Ruto katika kiwanda cha kusafidha mafuta mjini lagos nigeraia.

Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Lamu kinachofadhiliwa na Dangote kitaanza kujengwa rasmi Septemba 30, na kinatarajiwa kusafisha mapipa laki saba ya mafuta ghafi kwa siku punde kitakapokamilika.

Mradi huo utagharaimu kati ya shilingi trilioni 1.9 na trilioni 2.2 na utachukua kipindi cha hadi miaka mitatu kwa ujenzi wake kukamilika.

Share This Article