Taasisi za urekebishaji tabia zimekumbatia teknolojia kuimarisha utoaji huduma

Tom Mathinji
1 Min Read

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, amesema taasisi za urekebishaji tabia hapa nchini, zimekumbatia matumizi ya teknolojia, ili kufanikisha utoaji bora wa huduma.

Akizungumza Jumanne asubuhi wakati wa ufunguzi rasmi wa awamu ya nne ya wiki ya urekebishaji tabia Jijini Nairoobi, Kindiki alidokeza kuwa utumizi wa akili unde na teknoliojia zingine ibuka, zitapiga jeki utekelezaji wa mipango na kutambua mapemgo kwenye utoaji wa huduma na kufanikisha utumizi wa rasilimali chache kwenye taasisi hizo.

“Haya yanapaswa kutekelezwa huku tukizingatia maadili ya kibinadamu, ulinzi wa deta za kibinafsi na kudumisha haki na maswala ya walio chini ya uangalizi wa taasisi za urekebishaji tabia,” alisema Kindiki.

Kulingana na Kindiki, utumizi wa nishati safi, uvunaji na uhifadhi wa maji ya mvua, mbinu bora za kilimo, upanzi wa miti utajumuishwa ili kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Share This Article