Timu ya taifa ya soka ya Kenya,Harambee stars imeripoti kambini mapema Ijumaa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo kujiandaa kwa mechi ya kufuzu kwa AFCON mwaka 2027 dhidi ya Eritrea.
Wachezaji wa Harambee Stars walikuwa wamesusia mazoezi kuanzia mapema wiki hii wakidai kulipwa malimbikizi ya marupurupu ya mechi zilizopita .
Kenya inajiandaa kukabiliana na Eritrea katika mechi ya kwanza ya kundi D Jumamosi alasiri katika uwa wa kitaifa wa Nyayo kuanzia saa kumi .
Mataifa mengine katika kundi hilo na Kenya ni Afrika Kusini na Guinea.
Stars wanaofunzwa na kocha Benni McCarthy, wanatumia mechi hizo kujinoa kwa fainali za AFCON mwaka ujao,kwani tayari wamefuzu kama mojawapo wa waandalizi.
Fainali za 36 za AFCON zitaandaliwa kati ya Juni 19 na Julai 17 mwaka ujao katika mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania.