Rais William Ruto, aliye jijini New York nchini Marekani kuhudhuria Kongamano la 81 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) siku ya Alhamisi alifanya kikao na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani Gianni Infantino.
Ruto na Infantino walizungumzia ujenzi wa vituo vya ukuzaji vipaji nchini Kenya, kuimarisha soka ya mashinani na kuwa na mbinu mwafaka za viwango vya ukuzaji vipaji vya soka.
Ruto alikariri kuwa Kenya imewekeza pakubwa katika rasilimali za michezo, ikiwemo ujenzi wa viwanja 32 vipya katika kaunti mbalimbali nchini vya kiwango cha kimataifa.
Aidha, Rais aliweka bayana azma ya Kenya kuwa mstari wa mbele katika mataifa yanayowania maandalizi ya mashindano ya michezo ya kimataifa.