UNGA:Wajumbe waondoka ukumbini Netenyahu akihutubu

Licha ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivitita -ICC kutoa amri ya kukamatwa kwa Netenyahu  Novemba 21 mwaka 2024,bado kiongozi huyo yuko huru.

Dismas Otuke
1 Min Read

Baadhi ya wajumbe waliondoka nje ya ukumbi wa kongamano  la 81, la mkutano wa Umoja wa mataifa(UNGA), wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netenyahu, aliposimama kuhutubu .

Wajumbe hao waliteta hatua ya Israel kuvamia Wapelestina katika ukanda wa Gaza.

Nje ya ukumbi mjini New York,hali ilikuwa iyo hiyo mamia ya waandamanaji wakikamatwa na Polisi .

Waandamanaji hao walibeba mabango yaliyoitaka Marekani imkamate Netenyahu, kwa kutekeleza mauaji na ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu.

Licha ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivitita -ICC kutoa amri ya kukamatwa kwa Netenyahu  Novemba 21 mwaka 2024,bado kiongozi huyo yuko huru.

Hata hivyo ni vigumu kwa Marekani kumkamata  Netenyahu kwani Israel ni mshirika wa karibu wa Marekani.

 

Share This Article