Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen,ameagiza maafisa wa polisi wa akiba 8,000 wapewe mafunzo upya ili kuwawezesha kukabilaina na uhalisia wa changamoto za kisasa za kitaifa.
Akizungumza siku ya Jumatano katika chuo cha Magado katika hafla ya kufuzu kwa polisi wa akiba 705 kutokea kaunti kumi tofauti nchini,Murkomen alisema mafunzo ya awali kwa Polisi wa akiba yalijikita katika misingi ya kikabila na kimaeneo na hivyo kuwaweka polisi hao katika hali ngumu ya kufanya kazi nje ya maeneo yao.
Murkomen alisema mafunzo hayo yatawasaidia Polisi hao wa akiba katika utendekazi wao ,akiwaonya dhidi ya kutumia silaha wanazopewa kutekeleza uhalifu.
Aidha,aliwataka Polisi hao kuliwajibikia taifa badala ya wanasiasa wakati taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujo.