Benki Kuu ya Kenya yaadhimisha miaka 60 tangu kubuniwa

Rais Ruto alisifia jukumu muhimu la CBK kuhakikisha uthabiti wa kifedha nchini ikiwemo wakati wa kupanda kwa bei ya kubadilisha dola ya Marekani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Benki Kuu ya Kenya(CBK) iliadhimisha miaka 60 tangu kubuniwa kwake Alhamisi usiku katika hafla iliyohudhuriwa na William Ruto.

Hafla hiyo iliandaliwa katika Chuo cha Kutoa Mafunzo ya Usimamizi wa Fedha nchini kwenye barabara kuu ya Thika.

Rais Ruto alisifia jukumu muhimu la CBK kuhakikisha uthabiti wa kifedha nchini ikiwemo wakati wa kupanda kwa bei ya kubadilisha dola ya Marekani.

Aliongeza kuwa CBK imedhibiti bei hiyo ambapo kwa sasa dola moja inanuliwa kwa shilingi 129 huku mfumko wa bei za bidhaa ukisalia asilimia 6.6 katika mwezi wa Agosti.

Rais alitaja pia CBK imezisaidia benki za kibiashara kutoa mikopo kwa wateja wake ambayo imechangia kuimarika kwa maisha ya familia, kuongeza uwekezaji, kubuni nafasi za ajira na kukuza uchumi wa nchi.

Share This Article