Nimewasame wapinzani wangu wa kisiasa, asema Kindiki

Naibu huyo wa Rais aidha, alisisitiza kuwa serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo  katika kaunti ya Meru, ukiwemo upanuzi wa hospitali ya  Nyambene Level Four.

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, akiwahutubia wakazi wa Maua, kaunti ya Meru.

Naibu Rais  Prof. Kithure Kindiki, leo Alhamisi ametangaza kuwasamehe wapinzane wake wa kisiasa katika kaunti ya Meru, aliowataja wamekuwa wakiendeleza matusi na mashambulizi ya kibinafsi dhidi yake.

Akizungumza alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo katika eneo bunge la Igembe Kusini, kaunti ya Meru, Kindiki alidokeza kuwa hatajibu mashambulizi yao kwa matusi, badala yake ataangazia  utekelezaji wa miradi ya serikali na kuwahudumia wakazi wa Meru na taifa hili kwa jumla.

Naibu huyo wa Rais aidha, alisisitiza kuwa serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo  katika kaunti ya Meru, ukiwemo upanuzi wa hospitali ya  Nyambene Level Four, ujenzi wa masoko, barabara na uwanja wa  Maua uliopendekezwa.

Alitaja baadhi ya miradi ambayo serikali inatekeleza katika kaunti ya Meru ambayo inajumuisha, ujenzi wa kilomita 500 ya barabara ya safu mbili itakayogharimu shilingi bilioni 39, ujenzi w soko la kisasa kwa kitita cha shilngi bilioni 3 na kupandisha hadhi hospitali ya Nyambene Level 4 hadi kiwango cha Level 5.

Akiwahutubia wananchi Maua mjini, Kindiki alisema wakulima wanafurahia sana kupunguzwa kwa bei ya mbolea kutoka shilingi 7,000 hadi shilingi 2,000 na kupunguzwa kwa bei ya mbegu kutoka shilingi 300 hadi shilingi 150.

Share This Article