Mkenya anayetafutwa na Marekani anyimwa dhamana na mahakama

Kibutu ataendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri, akisubiri kusikilizwa kwa kesi kuhusu kurejeshwa kwake Marekani.

Tom Mathinji
1 Min Read
Sancho Kibutu.

Raia wa Kenya anayetafutwa na Marekani ili afunguliwe mashtaka kutoka na kosa la kuendesha gari akiwa mlevi, ataendelea kuzuiliwa korokoroni.

Hatua hii inajiri baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, kupinga ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana.

Sancho Kibutu, alikuwa ametuma ombi la kuachiliwa kwa dhamana, akisema atatii masharti atakayopewa, lakini mahakama ilikataa ombi hilo, huku akitaka apewe muda zaidi kujibu maombi ya kiongozi wa mashtaka ya kutaka apelekwe nchini Marekani, baada ya kupewa stakabadhi za kumrejesha Marekani.

Upande wa mashtaka ulipinga dhamana ukitaja uzito wa kesi hiyo, ombi la kurejeshwa nchini Marekani na hatua yake ya kukosa kuhudhuria vika vya mahakama nchini Marekani.

Kibutu ataendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri, akisubiri kusikilizwa kwa kesi kuhusu kurejeshwa kwake Marekani.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 25 Septemba 2026.

Share This Article