Rais Ruto: Sekta ya sukari imeimarika katika utawala wangu

Ruto amesema kuwa serikali itatenga ekari 300 za ukuzaji miwa huku nchini hii ikitarajiwa kuanza kuuza sukari nje ya nchi .

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amesema  serikali imestawisha na kuimarisha sekta ya sukari hapa nchini chini ya utawala wake wa miaka minne.

Akizungumza kwenye mahojiano ya moja kwa moja na Wanahabari katika kaunti ya Kisumu, Ruto amesema kuna usimamizi mpya katika viwanda vyote vya serikali vya kusaga miwa.

Aliongeza kuwa kinyume na awali wakulima wanaowasilisha miwa hulipwa kila wiki huku wanaocheleshwa sana wakipokea malipo yao ndani ya mwezi mmoja.

Rais ameongeza pia kuwa wafanyakazi ambao walikuwa wakicheleweshwa mishahara kwa sasa wanalipwa kwa wakati ufaao kila mwezi.

Amesema kuwa kwa sasa kuna viwanda vitano vipya vilivyosajiliwa maajuzi huku vingine vitatu vikitarajiwa kufunguliwa.

Ruto amesema kuwa serikali itatenga ekari 300 za ukuzaji miwa huku nchini hii ikitarajiwa kuanza kuuza sukari nje ya nchi .

Share This Article