IEBC yachapisha notisi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027

IEBC imetoa notisi hiyo ikiwa takriban mwezi mmoja baada ya kutoa kalenda ya uchaguzi kuanzia kwa uteuzi,kipindi cha kampeni hadi kuelekea debeni.

Dismas Otuke
1 Min Read
Erastus Ethekon - Mwenyekiti wa IEBC

Tume huru ya mipaka na uchaguzi nchini Kenya,IEBC imechapisha notisi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 ulioratibiwa kuandaliwa Agosti 10 .

IEBC imetoa notisi hiyo ikiwa takriban mwezi mmoja baada ya kutoa kalenda ya uchaguzi kuanzia kwa uteuzi,kipindi cha kampeni hadi kuelekea debeni.

Aidha,notisi hiyo inajumuisha mpangilio na ratiba ya kuelekea uchaguzi mkuu ,ikiwemo uteuzi wa vyama,masharti ya uteuzi kwa waaniaji katika nyadhifa mbalimbali.

Pia mpangilio huo unajumuisha masharti ya kifedha yanayohitajika kwa waaniaji mbalimbali.

Maafisa wa umma wanaonuia kuwania viti katika uchaguzi mkuu wa mwaka  ujao ni sharti wajiuzulu kufikia Februari 9, mwaka ujao,ikiwa miezi sita kabla ya siku ya uchaguzi mkuu.

Share This Article