Kesi ya Lissu kuendelea leo

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche atakabiliwa na maswali ya dodoso kutoka upande wa mashtaka.

Marion Bosire
1 Min Read
John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara

Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA inatarajiwa kuendelea leo Jumatatu Septemba 14, 2026.

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche atakabiliwa na maswali ya dodoso kutoka upande wa mashtaka.

Hatua hiyo inafuatia ile ya Heche kukamilisha kutoa ushahidi wake mbele ya Mahakama, Ijumaa iliyopita akieleza mambo mbalimbali kuhusu mkutano wa CHADEMA wa Aprili 3, 2025, ambao umehusishwa na kauli zinazounda sehemu ya mashtaka dhidi ya Lissu.

Heche aliieleza Mahakama kuwa Lissu hakuhusika katika maandalizi ya mkutano huo, bali alialikwa kama Mgeni Rasmi na mzungumzaji mkuu. Alisema kauli za Lissu kuhusu kuzuia au kuvuruga uchaguzi zilihusu kutumia njia za kidemokrasia.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Heche alisema Lissu hakuwa na nafasi katika matukio yaliyotokea siku hiyo kwa kuwa tayari alikuwa amekamatwa.

Baada ya Heche kumaliza ushahidi wake, Mahakama iliruhusu upande wa mashtaka kuanza kumuuliza maswali ya dodoso, lakini Wakili Mkuu wa Serikali, Nassor Katuga, akaomba kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi leo, akieleza kuwa wana maswali mengi kutokana na ushahidi uliotolewa na shahidi huyo.

Share This Article