Maambukizi ya Ebola nchini DRC yafikia visa 7,000

Haya yanajiri licha ya taifa hilo la Afrika Mashariki kuanza kutoa chanjo ya kitaifa ya Ebola ili kuzuia maambukizi mapya.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola yamefikia visa 7,000 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC huku idadi ya waliofariki ikifikia 3,398.

Kulingana na ripoti za serikali ya DRC, jumla ya watu 7138 wameripoitiwa kufariki kufikia Ijumaa iliyopita kutokana na virusi vya Bundibugyo.

Aidha, idadi ya mikoa iliyoripoti maambukizi imeongezeka hadi saba, mkoa wa hivi punde ukiwa South Ubangi.

Haya yanajiri licha ya taifa hilo la Afrika Mashariki kuanza kutoa chanjo ya kitaifa ya Ebola ili kuzuia maambukizi mapya.

TAGGED:
Share This Article