Nairobi kati ya kaunti zitakazopokea mvua kwa siku 5 zijazo

Kakamega, Bungoma, Vihiga, Busia, Kisumu, Siaya, Homa Bay na Migori zinatarajiwa kupata mvua alasiri kuanzia Jumapili hadi Jumanne.

Marion Bosire
1 Min Read

Nairobi ni moja ya kaunti kadhaa nchini Kenya zinazotarajiwa kupokea mvua katika kipindi cha siku tano zijazo, huku Mamlaka ya Hali ya Hewa Kenya ikiwataka wakazi kujiandaa kwa mvua ya wastani hadi kubwa.

Utabiri huo unahusu kipindi cha Jumapili, Septemba 13 hadi Alhamisi, Septemba 17, 2026. Mvua nyingi inatarajiwa kunyesha alasiri, ingawa baadhi ya maeneo yanaweza kupata mvua za asubuhi.

Nairobi, Kiambu, Meru, Tharaka Nithi, Nyeri na Murang’a, zinatarajiwa kupata mvua kuanzia Jumapili hadi Jumatano.

Nyandarua pia itapata mvua nyakati za alasiri Jumapili, Jumatatu, Jumatano na Alhamisi, huku Kirinyaga ikitarajiwa kupata mvua nyepesi Jumapili, Jumatano na Alhamisi.

Magharibi mwa Kenya na maeneo ya Bonde la Ziwa Victoria pia yanatarajiwa kupata mvua. Kakamega, Bungoma, Vihiga, Busia, Kisumu, Siaya, Homa Bay na Migori zinatarajiwa kupata mvua alasiri kuanzia Jumapili hadi Jumanne.

Kaunti za Pwani, zikiwemo Mombasa, Kwale, Lamu, Kilifi na Taita Taveta, zitapata vipindi vya mvua, huku baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa Kenya yakitarajiwa kupata mvua nyepesi alasiri.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini pia imeonya kuhusu usiku wenye baridi katika kaunti kadhaa. Nairobi inatarajiwa kuwa na joto la chini la kati ya nyuzi 12 na 15, huku Nyandarua na Samburu zikitarajiwa kushuka hadi nyuzi 6.

Share This Article