Rais William Ruto ameendeleza ziara yake katika eneo la South Rift huku akifungua na kukagua miradi kadhaa ya maendeleo.
Mapema Jumamosi Ruto aliweka jiwe la msingi ,ujenzi wa hospitali ya Chebunyo Mother and Child Hospital,kaunti ya Bomet.
Hospitali hiyo ya Level 4 itakuwa na vitanda 250 na itatoa huduma za afya ya kina mama na kujifungua na pia matibabu ya watoto.
Hospitali hiyo inajengwa na kampuni ya Amsons Group kwa kima cha shilingi bilioni 4.5, chini ya mradi wa Mama na Mtoto Kwanza.
Aidha, rais amezindua miradi ya ujenzi wa barabara ra Mid-West Chelimo kaunti ya Kericho na kukagua ujenzi wa soko la kisasa la Chebunyo na pia mradi wa uunganishaji umeme wa Chepalungu kaunti ya Bomet.