Wanawake wahimizwa kutumia fursa za serikali kuimarisha mapato

Mama Taifa alidokeza kuwa mradi wa kitaifa wa kuimarisha mfumo wa kuongeza thamani bidhaa za kilimo (NAVCDP), huenda ukaimarisha hali ya wakulima wa mashamba madogo madogo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rachel Ruto - Mama Taifa.

Mama wa taifa Rachel Ruto ametoa wito kwa wanawake nchini Kenya, wachukue fursa za serikali zilizoko hasaa katika sekta ya kilimo ili kuimarisha mapato na kubuni riziki endelevu.

Alisema serikali inawezeka katika masoko, kuimarisha mifumo ya kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo na kuimarisha upatikanaji wa mikopo ya riba nafuu ili kuwawezesha wakulima hasa wanawake kukuza biashara zao.

Akizungumza Ijumaa katika kaunti ya Vihiga, Mama Taifa alidokeza kuwa mradi wa kitaifa wa kuimarisha mfumo wa kuongeza thamani bidhaa za kilimo (NAVCDP), huenda ukaimarisha hali ya wakulima wa mashamba madogo madogo kwa kuwahimiza kujihusisha katika kilimo cha mimea muhimu zikiwmeo ndizi, kuku, ufugaji ng’ombe wa maziwa, mboga za kiafrika na parachichi.

“Mwanzo mdogo unauwezo wa kuleta mafanikio makubwa iwapo wanawake watachagua kushirikiana pamoja,” alisema Mama Taifa.

Alisema  makundi ya wanawake pia yanaweza kunufaika kutokana na ruzuku na fursa za ustawi wa biashara huku shirika la wanawake la Joyful likiwaandaa wanawake kuchukua fursa hizo kupiti

Share This Article