Brazil wamedumisha rekodi ya asilimia 100 baada ya kuibwaga Uingereza mabao 2-1, na kuongoa kundi B kwa alama 9 ,katika fainali za Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 20 nchini Poland.
Katika mechi nyingine Canada iliweka hai matumaini ya kufuzu kwa raundi ya mwondoano baada ya kuigaragaza Tanzania 6-0, wakati Uingereza pia ikimaliza ya pili kundini na kujikatia tiketi.
Wenyeji Poland na Italia pia wamefuzu kwa hatua ya mchujo.
Afrika inawakilishwa na Nigeria,Tanzania,Ghana na Benin katika fainali hizo.
Jumla ya mataifa 24 yanashiriki kipute hicho huku fainali ikipigwa Septemba 27.